Na Mwandishi Wetu. Unguja
Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC imeshindwa kuondoka na ushindi baada ya kulazimishwa sare tasa 0-0 na wachovu wa Yanga, Mlandege FC mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mlandege ambao juzi walipokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga ambao kwa sasa wameenda Pemba, waliweza kuwadhibiti vilivyo Simba ambao walichezesha kikosi chao chote lakini kikashindwa kufurukuta.
Simba wameweka kambi yao kisiwani hapa wakijiandaa kucheza na Yanga hapo Jumatano ijayo katika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuwania Ngao ya Jamii, matokeo hayo yanawashangaza wengi kwani baada ya Mlandege kufungwa na Yanga washabiki wa Simba walikuwa wakiibeza Mlandege wakidai ni vibonde