Msuva aitosa Yanga, atua Mbao FC

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kiungo James Happygod Msuva amejiunga na Mbao FC ya Mwanza baada ya kuachana na Yanga SC aliyoitumikia kwa vipindi kadhaa.

James ni mdogo wa winga wa Yanga na Taifa Stars, Simon Msuva ambaye kwa sasa yupo kwenye ubora wake.

Kiungo huyo amejiunga na Mbao na msimu ujao ataitumikia timu hiyo, awali Msuva aliwahi kuzichezea Simba SC na Azam zote zikiwa timu za vijana

James Msuva, ameihama Yanga
James (Kushoto, akiwa na kaka yake, Simon, wote hao wameihama Yanga