KABURU HOI MAHABUSU, AVEVA AJITOKEZA KISUTU

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' yuko hoi mahututi na amelazwa katika hospitali ya Keko inayomilikiwa na gereza la Keko ambako yeye na mwenzake Evans Aveva wanashikiliwa.

Kaburu leo hakutokea mahakamani ambako wamehitajika kwa ajili ya kusikiliza shauri lililo mbele yao likihusu utakatishaji fedha, Rais wa klabu hiyo Evans Aveva alijitokeza mahakamani hapo ila Kaburu hakutokea.

Wawili hao sasa wataendelea kusota rumande hadi Julai 31 watakaudhuria tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako ndiko inakosomwa kesi yao, wawili hao walikamatwa tangu Juni 29 mwaka huu wakituhumiwa kwa makosa matano

Evans Aveva ametokea mahakamani Kisutu leo, lakini mwenzake Kaburu hakutokea