Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Manara amnanga Mbolembole

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Afisa Habari aliyesimamishwa wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amemvaa blogger wa tovuti ya Shafih Dauda, Baraka Mbolembole na kumwambia aache kuiandika vibaya Simba kila anapokurupuka.

Manara amesema kuwa Mbolembole ana tabia ya kuiandika vibaya Simba hata kama inafanya vizuri, Akiandika jana kwenye ukurasa wake wa Twitter, Manara amefunguka mengi akianza kumsifu Shafih Dauda anayefanya kazi yake Clouds Media kupitia redio na televisheni.

Shafih Daud ni mmoja ktk watu wa soka hapa nchini,ni rafiki yangu tunaoongea muda mrefu hususan masuala ya mchezo huu murua,uliyobeba maisha yangu,pia ni kijana mwenzangu tunaoheshimiana sana,kiasi cha kwamba sijawahi kwa namna yoyote ile kukwazana nae,hata kama tunatofautiana kimtazamo ktk baadhi ya mambo, hususan ya Soka.

Wengi mnakumbuka sakata la Ramadhan Singano,jinsi lilivyokaribia kuvunja uhusiano wetu,kwa jinsi alivyolivalia njuga bila kuujua ukweli,lakini mwishoe ni yy juzi tu aliandika kuwa Singano anataka kuvunja mkataba wake ambao hadi sasa naamini c HALALI, mkataba ulioidhinishwa na TFF huku akiwa na mkataba na klabu nnayoisemea na kuishabikia Simba SC, lakini hayo yashapita, udugu na uhusiano wetu bado upo pale pale.

Hata jana baba yangu mdogo Kassim Manara, aliyepo nchini kwa likizo ya majira ya kiangazi toka aishipo huko Belgium, alitaka kuongea nae kupitia cm yangu,na waliongea mengi, huku akimsifu ni kijana mstaraabu ambae hajawah kukosa kwenda kumsalimia pale Antwerp kule Belgium ama Belige kama waitavyo wacongo,kila apatapo nafasi ya kwenda huko, hakika huyu na Eddo kumwembe ni washabiki wakubwa wa wazee wangu, Sunday na Kassim Manara, hata Eddo alimtembelea mwanasoka huyo mahiri wa zamani na wa kwanza nchini kutikisa nyavu za Santiago Barnabeu,wakati akicheza soka la kulipwa kule Austria.

Lakini leo nimeamua kumwambia ukweli *'swahiba'* wangu huyo, ukweli ambao ninaamini ataufanyia kazi kwa haraka,ili kulinda image yake na ya blog anayoiongoza na iliyo maarufu miongoni mwa blogs za michezo nchini.

Asubuhi nilimpigia kumweleza dukuduku langu, juu ya makala zinazoichafua klabu na uongozi wa Simba, znazoandikwa na mtu aitwae *Mbolembole*, mtu huyu ni mgeni ktk Soka, simjui,sina rekodi nae zozote, ama za uandishi wa michezo, au hata uchambuzi kama walivyo Shafih na kina Eddo.

Mtu huyu kila kukicha huandika vtu vbaya kuhusu Simba, hutuchokoza na kutaka kuaminisha watu Simba ni klabu ya hovyo na inaongozwa na watu wasiojua lolote kuhusu futboll.

Anaitumia blog ya Shafih kuidhalilisha klabu yetu na hata wachezaji wa klabu, hutumia pia blog hii kujipatia umaarufu *KUNUKA* kwa kuisanifu Simba.

Nimemvumilia vya kutosha sana, najua hana hadhi wala heshma ya kujibiwa na mm, ila kwa kuwa anatumia blog ya mtu niliye na uhusiano nae mzuri na wa muda mrefu,inabidi ajibiwe tu,no matter kama kumjibu huku atajipatia umaarufu wa muda mfupi.

Ameandika ktk makala yake kuwa *Usajili wa hv sasa wa Simba ni anguko lingine*, na akadai Simba haijalipa wachezaji wake mishahara ya mwezi wa tano,na pia *usajili huu hautokani na ripoti ya Kocha Omog.*

Hv iwe ni kweli klabu haijalipa mishahara ya mwezi wa tano,tatizo lipo wapi? hv kuchelewesha mshahara wa mwezi mmoja kwa klabu za Tanzania ni Ishu?na nani kamwambia kuwa hatujalipwa mishahara!!anaweza kuweka ushahidi? pili hilo anguko kwa kumsajili Okwi au kapombe?na hyo ripoti ya Omog kaiona wapi?kwao Mbwinde au!!

Labda nimpashe usajili wa kapombe, Boko na Manula ni matakwa ya mwalimu,ni wachezaji anaowajua vema toka akiwa kocha wa Azam,na umelenga kukiimarisha kikosi chetu kwa ajili ya michuano ya kimataifa,ambayo mwakani tunashiriki.

Hatukusajili kwa fashen, tumesajili kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu,na hakuna mahali kokote Omog kamtaja Ndikumana,na kama kwa kumtaja kwake anadhani tutamsajili ili apate cha juu,imekula kwake,hana nafasi Simba, na nimwambie hao wote ni trela,kishindo kikuu kipo njiani.
Ameandika pia *Simba haijaandika lolote FIFA,* nimwambie tu kuwa chombo hicho huwa hakikurupuki ktk kufanya maamuzi yake, kinafanya uchunguzi makini kabla ya kufanya maamuzi,na asubiri aone majibu yao,ndio aropoke USHUZI wake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC