Thomas Ulimwengu aanguka miaka miwili Sweden

Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu amesaini mkataba was miaka miwili kujiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Sweden ya AFC eskilstuna iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.

Ulimwengu amejiunga na timu hiyo baada ya kusota kwa muda mrefu tangu alipoachana na timu yake ya TP Mazembe ya DR Congo aliyoiongoza kuipa mataji ya Ligi ya kwao na Afrika.

Mshambuliaji huyo amefuata nyayo za Watanzania wenzake Athuman Machupa, Shehan Rashid, Joseph Kaniki na Haruna Moshi ambao wamewahi kucheza Sweden, hata hivyo meneja wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amesema kutua Sweden kwa nyota huyo hakuna maana kwamba amefeli.

Anadai Ulimwengu alipata ofa mbalimbali Ubelgiji, Ufaransa, Italia, Hispania lakini hakuna hata timu moja iliyokuwa 'Serious' kumchukua, hivyo Ulimwengu kutua Sweden si kwamba amefeli bali amekwenda kuimarisha kiwango chake ili ajiandae kwenda juu zaidi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI