Na Prince Hoza, Zanzibar
Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza leo katika uwanja wa Amaan Zanzibar, mchezo wa ufunguzi utapigwa usiku saa 2:00 kati ya watani wa jadi Taifa Jang' ombe na ndugu zao Jang' ombe Boys.
Wakati leo ukifanyika ufunguzi, kesho kutwa tarehe 1 January 2017 kutapigwa mechi mbili, jioni saa 10:00 KVZ ya Zanzibar itachuana na mabingwa watetezi URA ya Uganda na kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Taifa Jang' ombe