Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: YANGA TAMBUENI LWANDAMINA SIYO MALAIKA

Na Prince Hoza.

YANGA SC wanataka kufanya mabadiliko makubwa ya benchi lake la ufundi ili mradi waweze kurejesha makali yao mapya yaliyopotea katika siku za hivi karibuni, tayari jina la kocha mpya limeshajulikana na awali aliwahi kutua hapa nchini kuzungumza na mabosi wa timu hiyo.

Mzambia George Lwandamina ndiye jina la kocha mpya wa Yanga anayetajwa kwenye vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya kijamii, Mzambia huyo alianza kuzungumziwa miezi kadhaa iliyopita hadi kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans Van der Pluijm akaamua kujiuzuru.

Magazeti ya Tanzania hayakuficha yaliandika kila kitu, Mholanzi huyo alikasirishwa na kitendo hicho cha mabosi wa Yanga kuamua kumletea kocha mwingine wakati yeye anafanya vizuri, yaliyokuwa yakisemwa yote Babu Hans aliyaona hivyo akajipanga kuwasubiri viongozi wa Yanga wamfuate.

Viongozi wa Yanga walipendekeza Lwandamina awe kocha mkuu na Babu Hans awe mkurugenzi wa ufundi, na walipomfuata kumpa taarifa hizo Babu akawatolea nje akaamua kubwaga manyanga na kutaka kurejea kwao Ghana, kocha huyo anaishi nchini Ghana.

Baada ya Hans kujiuzuru ukocha, mwanachama mwenye ushawishi mkubwa wa Yanga, Mhe Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Waziri wq Mambo ya Ndani ya nchi, akaamua kumfuata Babu Hans na kumbembeleza asalie Yanga, kisha akawafuata viongozi wa Yanga na kuwaomba wambakishe Babu Hans na wamuombe radhi kwa kile walichotaka kukifanya.

Ni kweli uongozi wa Yanga ulimuonba radhi Babu Hans na baadaye kocha huyo akatangaza kurejea kazini, Kilichomfanya Mwigulu amfuate Babu Hans ni kutokana na rekodi zake ndani ya Yanga, Mholanzi huyo tangu alipotua Yanga kwa mara ya kwanza kwa kipindi kifupi cha miezi sita alilibadili soka la Wanajangwani hao ambao walikuwa wakitoa dozi.

Ushindi wa mabao 7-0 mpaka 8-0 ulikuwa kama jadi kwani vijana hao wa Yanga walikuwa wakizifunga timu mbalimbali idadi hiyo ya mabao, kocha huyo aliondoka Yanga kisha akarejea tena kwa mara ya pili ambapo aliwapa Yanga ubingwa wa Bara mara mbili mfululizo, pia akawapa Ngao ya Jamii mara mbili na kombe la FA.

Pluijm akaiwezesha Yanga kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika ingawa haikufanya vizuri, hata hivyo Yanga ilipangwa kwenye kundi gumu ambalo lilitoa timu mbili zilizocheza fainali ambazo ni TP Mazembe na Mo Bejaia.

Yanga kwa sasa wanacheza kandanda zuri na la hali ya juu hivyo kocha huyo anastahili kuendelea kukinoa kikosi hicho cha Wanajangwani, Pia Yanga ikaweza kuifunga Simba mechi zote mbili mfululizo za Ligi kuu Bara.

Kwa kifupi Pluijm amezima ngebe zote za Simba, kitendo cha uongozi wa Yanga cha kutaka kumfukuza kocha huyo kilichukuliwa kama cha kutaka kuiua timu hiyo, Mhe Mwigulu akaona Yanga itapotea na atakosa furaha, maana Mwigulu amechoka kuzomewa na watani zake Simba hivyo kwa kujumlisha rekodi za Babu Hans akaona bora abakie kwa nguvu zote.

Lakini kiukweli Yanga hii na hasa ya msimu huu imepoteza mwelekeo, Yanga imeachwa nyuma na mtani wake Simba kwa tofauti ya pointi tano, Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 35 kwa mechi 14 wakati Yanga wanashika nafasi ya pili na pointi 30 kwa mechi 14.

Inawauma sana Wanayanga kukaa nafasi hiyo isitoshe wao wanajiita Wakimataifa, Yanga nafasi hiyo hawaitaki, ingawa ilionekana tangu maoema kwamba Yanga haitafanya vizuri msimu huu kwakuwa wachezaji wake hawajapa mapumziko yoyote, kikosi cha Yanga kilishiriki mashindano mbalimbali pasipo kupumzika hivyo wengi wao wameanza kuchoka.

Mchezaji kama.Thabani Kamusoko si yuke wa msimu uliopita ambaye alikubalika mno mpaka kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, hata makali ya Donald Ngoma si yale ya msimu uliopita, kwa sasa Ngoma amepungua, hilo nalo linan
mkwamisha Pluijm.

Mwenyekiti wa timu hiyo Yusuph Mehbood Manji ameamua kusitisha ajira ya Pluijm na kushikilia msimamo wake wa kumleta Mzambia Lwandamina, Tayari taarifa za kuja kuanza kazi Mzambia huyo zimeshazagaa jijini na barua ya kujizuru kwenye timu yake ya Zesco zimeshaonekana mitandaoni.

Lwandamina anakuja kurithi mikoba ya Pluijm lakini pia kuna tetesi ya kuondoshwa benchi lote la ufundi, Yanga wanataka kuwaondoa Juma Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi, Juma Pondamali ambaye ni kocha wa makipa na Hafidh Saleh ambaye ni meneja.

Fununu zinaeleza kwamba Cherles Boniface Mkwasa ambaye ni kocha mkuu wa Taifa Stars, anakuja kuwa kocha msaidizi wa Yanga, Peter Manyika anakuwa kocha wa makipa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Sekilojo Jonson Chambua anakuwa meneja.

Mabadiliko hayo kwa vyovyote yataanza mzunguko wa pili ambapo Yanga watakuwa wakisaka ubingwa wa bara, Wengi wanaamini Yanga ikiwa na sura mpya kwenye benchi la ufundi wataweza kufanya vizuri ikiwemo kutwaa ubingwa wa bara, Lakini hiyo si kazi nyeoesi kwani ligi ya msimu huu inaonekana ni ngumu mno, kila timu inataka kuchukua ubingwa, na nyingine kujinusuru kushuka daraja hivyo ugumu unaonekana mapema.

Makocha wapya hawawezi kuibadili timu haraka na mpaka ikachukua kikombe, ninachoona hapo huenda kikosi cha Yanga kikafumuliwa nakujengwa upya, madhara ya kujenga kikosi upya ni makubwa, timu itacheza bila kuzoeana kwani kila kocha ana chaguo lake, Yanga wakubaliane na hali yoyote ile na wasitegemee kama Lwandamina amekuja na jipya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC