Yanga yaichanachana Mbao

Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Bara, Yanga SC, jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru imeichanachana vibaya Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 3-0 mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mbao ambayo ilichapwa bao 1-0 na Simba katika dakika za mwisho mpira kumalizika leo nayo ilikataa kuruhusu bao kipindi cha kwanza ambapo walienda mapumziko wakiwa suluhu, kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Vincent Bossou ambaye ni beki wa kati.

Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na mlinzi wa kulia ambaye pia hucheza nafasi zote za ulinzi Mbuyu Twite aliyeurusha mpira ulioingia wavuni ukiguswa na kipa wa Mbao  Amissi Tambwe aliongeza bao lake la saba na la tatu kwa Yanga.

Kwa matokeo ya mcheo wa leo Yanga imefikisha pointi 27 huku ikiendelea kuifukuzia Simba inayoongoza Ligi ikiwa na pointi 32