Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC, jioni ya leo imeilaza Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa jumla ya mabao 3-1 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga iliyotoka kwenye matokeo mabaya ya kulazimishwa sare ya 1-1 na watani zao Simba, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mzambia, Obrey Chirwa ambaye leo ndio ametoa mkosi kwa kufunga bao lake la kwanza.
Mtibwa Sugar ilisawazisha bao hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa winga wake Haroun Chanongo, lakini wakazinduka na kuongeza bao la pili likifungwa na Simon Msuva kisha ikaongeza la tatu likifungwa na Donald Ngoma.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 14 ikiwa imecheza mechi saba, mechi nyingine kama ifuatavyo, Stand United 1 Azam FC 0, Mbao 3 Toto Africans 1