Na Saida Salum, Dar es Salaam
Imefahamika kwamba waamuzi wote wanaochezesha mechi za Ligi kuu Bara na Ligi Daraja la kwanza Tanzania bara, wamepanga kugomea kuchezesha mechi zote za Coastal Union ya Tanga kufuatia mashabiki wa timu kuwa na tabia ya kuwapiga na kuwajeruhi waamuzi.
Hiyo imefahamika hasa kufuatia mashabiki wa Coastal kujitokeza uwanjani na kumpiga vibaya mwamuzi aliyekuwa akichezesha mechi yao na kumdhuru, Video iliyoenea mtandaoni ikimuonyesha mwamuzi aliyekuwa akichezesha mechi ya Coastal Union akipigwa na mashabiki wa Coastal.
Licha ya mashabiki hao kutumia viti na chupa za maji kumpiga mwamuzi huyo aliyekuwa akiamuliwa na polisi mmoja ambaye naye alielemewa na kundi kubwa la mashabiki hao wahuni wa Coastal waliojifanya wana hasira kali, waamuzi wamesema hawatachezesha mechi za Coastal na wanashinikiza timu hiyo ifutwe