Thomas Mashali auawa Dar

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana huko maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana ambazo zona uhakika zinasema Mashali alipigwa na watu waliokuwa na silaha za jadi ambao walidhani mwizi.

Rafiki wa karibu wa bondia huyo aliyepata kutamba hapa nchini amesema marehemu hakuwa na tabia ya wizi, anasema huenda watu waliompiga walidhania mwizi ama baadhi ya watu wanaomfahamu walimwita mwizi ili apigwe hadi kufa.

Rafiki huyo alizungumza huku akilia amedai Mashali ni mtu safi na wala hakuwa tabia ya ukorofi, lakini kuna taarifa nyingine inasema Mashali alikuwa kwenye ugomvi na wenzake hivyo aliwazidi nguvu na ndio maana wakamwitia mwizi na kupelekea kupigwa hadi kufa, maiti yake iliokotwa na waendesha bodaboda