Na Saida Salum
Vinara wa Ligi kuu Tanzania bara, Simba SC, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Mbeya.
Ibrahim Ajibu alikuwa wa kwanza kuifungia bao Simba, kabla ya Shiza Ramadhan Kichuya kuongeza bao la pili, Hata hivyo Simba walikosa penalti iliyopigwa na Fredrick Blagnon.
Kwa ushindi huo Simba inaendelea kujikita kileleni ikiwa na pointi 20 ikiwa imeshuka dimbani mara 8, Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo wao mwingine dhidi ya Prisons pia ya Mbeya.
Nayo Mbao FC imeichapa Toto Africans mabao 3-1 katika uwanja wa CCM Kirumba