Simba waiomba radhi serikali

Na Prince Hoza

Uongozi wa Klabu ya Simba, leo umetangaza kuiomba radhi serikalj ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya rais John Pombe Magufuli kwa kitendo cha mashabiki wake kung' oa viti vya uwanja wa Taifa, Dar es Sakaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara, amesema leo kwamba Klabu ya Simba inaiomba radhi serikalj kufuatia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na mashabiki wake.

Manara amedai serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuuendesha uwanja huo hivyo uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba hautavumilika, aidha Manara ameiomba serikali kuwapa tena nafasi ya kuutumia uwanja huo.

Wakati huo huo Klabu ya Simba leo imetangaza kamati mbalimbali ambazo zitahakikisha mnyama msimu huu ananyakua ubingwa wa bara baada ya misimu minne kuukosa, moja kati ya waliotangazwa kwenye kamati hizo ni Hassan Hasanoo, Juma Pinto na wengineo