Simba SC kuendeleza mauaji leo Uhuru

Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam

Vinara wa Ligi kuu bara, Simba SC, jioni ya leo inashuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Wanamkurukumbi, Kagera Sugar kutoka Misenyi mkoani Kagera mchezo wa Ligi kuu bara.

Mchezo huo utakuwa mkali kwakuwa kila timu inataka kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri, Simba ambao ndio wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 20 wana uhakika mkubwa wa ushindi kutokana na wachezaji wake kucheza kwa kujituma.

Shiza Kichuya ambaye ndiye kinara wa mabao kwa sasa akiwa amefunga mabao sita, anatarajia kuiongoza Simba leo katika mchezo huo wa tisa, Lakini mechi nyingine zitapigwa leo ambapo JKT Ruvu na Mwadui FC, Toto Africans na Majimaji, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons wakati Stand United itachuana na African Lyon