Simba na Yanga vitani tena leo

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, inatimua vumbi tena leo kwa miamba ya soka nchini Simba na Yanga kujitupa katika viwanja tofauti kuwania pointi tatu muhimu.

Miamba hiyo ina kumbukumbu ya kutoka sare ya 1-1 wao kwa wao juma lililopita katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga leo watawaalika wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiongoza na pointi zao 17 wakati Yanga wanashika nafasi ya sita na pointi zake 11