Simba kuwafuata Mbeya City

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Vinara wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Jumamosi wanaanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya ikiwa tayari kabisa kwa mecho zake mbili dhidi ya Mbeya City itakayocjezwa juma lijalo na mwingine dhidi ya Prisons.

Kocha mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog ameamua kuondoka na kikosi chake chote na ameahidi kupata pointi sita ingawa kocha msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso ambaye aliwahi kuichezea Simba miaka iliyopita amedai Mbeya City ni kiboko ya Julio hivyo Simba waangalie wanaweza kukwama mbele yao