Samatta atajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora Afrika

Na Mwandishj Wetu

Mtanzania Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya majina 30 yatakayowania tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa mwaka 2016 huku Yaya Toure akiachwa.

Katika orodha hiyo wamo wachezaji wengine ambao ni Riyad Mahrez, Pierre-Emerick Aubameyang na Kelechi Iheanacho.

Kutoka Afrika ya Mashariki pia wamo Victor Wanyama wa Kenya na Dennis Onyango wa Uganda.