Na Mwandishi Wetu
Kocha mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema yeye ndiye kocha mkuu wa Yanga na atambui kama kuna kocha mwingine atakuja kuinoa timu hiyo kwakuwa mpaka sasa hajapewa barua na mwajiri wake ya kuachishwa kazi.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Pluijm ameshangazqa na taarifa zilizosambaa kwenye kurasa mbalimbali za magazeti ya juzi na jana kwamba kuna kocha mpya anakuja kuchukua nafasi yake.
Mholanzi huyo aliyeinoa Yanga kwa misimu miwili na kuipa taji mara mbili mfululizo la Ligi kuu bara, ameweka rekodi ya kufundisha Yanga kwa miezi 12 akicheza mechi 54 huku akipoteza mechi saba tu kitendo kinachodaiwa ni heshima kubwa mno kuwekwa, hivyo kocha mpya atakuwa na kazi kubwa ya kuivunja rekodi yake.
Jana jina la Mzambia George Lwandamina ambaye ni kocha wa Zesco ametajwa kujiunga na Yanga akichukua nafasi ya Mholanzi huyo