Pluijm arejeshwa kinguvu Yanga

Na Mrisho Hassan

Baada ya kutangaza kujiuzuru kuinoa Klabu ya Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm amerejeshwa kinguvu leo katika Klabu hiyo na Waziri wa mambo ya ndani Mhe Mwigulu Nchemba ambaye ni mpenzi mkubwa na shabiki namba moja wa timu hiyo.

Taarifa za ndani zenye uhakika zinasema Pluijm ameombwa kurejea Yanga na mheshimiwa Mwigulu kwa vile ameiwezesha Yanga kufanya mambo makubwa katika kipindi chake alichoinoa timu hiyo, waziri huyo alizungumza na uongozi wa Yanga na kuwataka wamrejeshe haraka Mholanzi huyo kisha akazungumza na kocha huyo ili akubali kurejea Yanga.

Tayari Mholanzi huyo ameombwa radhi na viongozi wa Yanga na huenda leo akaanza kusimamia mazoezi ya mwisho ya timu hiyo ambayo Jumapili itacheza na Mbao FC, mchezo wa Ligi kuu Bara, Pluijm ameipa Yanga mataji mawili ya Ligi kuu Bara, taji moja la kombe la FA na kuifikisha Yanga hatua ya makundi kombea Shirikisho barani Afrika