Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Kiungo Muzamiru Yassin amelizamisha jahazi la timu ya Mbao FC kutoka Mwanza katika mchezo wa Ligi kuu Bara uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati Simba SC iliposhinda bao 1-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya ubingwa.
Vinara hao walijipatia bao hilo katika dakika za lala salama na kuamsha ndelemo kwa mashsbiki wake walioanza kukata tamaa kutokana na wapinzani wao Mbao kuonyesha kandanda safi huku mabeki.wake wakiwa makini kuwazuia washambuliaji wa Simba.
Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu walishindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa Mbao na kujikuta wanashindwa kufumania nyavu kama ilivyo kawaida yao, Shiza Kichuya naye alibanwa, Fredrick Blagnon ndiye aliyeingia na kubadili sura ya mchezo na Simba kupata bao la usiku.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 26 ikiwa imecheza mechi tisa na ikimuacha mtani wake Yanga kwa tofauti ya pointi 8