Muzamiru azamisha jahazi la Mbao usiku

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Jahazi la Mbao FC limezamishwa na kiungo Muzamiru Yassin katika dakika ya 86 na kuipa ushindi wa bao 1-0 Simba SC na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya Tanzania bara, katika mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mpambano huo ulikuwa mkali na wa kusisimua hasa kutokana na timu zote mbili kila moja ikitaka kuibuka na ushindi lakini bila mafanikio yoyote, hadi mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba wakionekana kulishambulia lango la Mbao lakini uimara wa mabeki wa Mbao uliwafanya Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo kushindwa kufunga.

Kuingia kwa Fredrick Blagnon kulileta mabadiliko katika safu ya ushambuliaji ya Simba na kulitia msukosuko lango la Mbao na hatimaye kiungo Muzamiry Yassin kuandikisha goli la ushindi ambalo limeipa Simba pointi tatu muhimu na kufikisha pointi 26 ikizidi kukaa kileleni na kumuacha hasimu wake Yanga kwa tofauti ya pointi nane