Mtangazaji wa BBC awa meneja Azam

Na Mwandishi Wetu

Mtangazaji wa zamani wa idhaa ya kiswahili wa Shirika la Utangazaji la BBC, Abdul Mohamed ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya Azam FC ya Dar es Salaam.

Uteuzi huo ulioanza Oktoba 1, mwaka huu ni sehemu ya mikakati ya Azam Fc ya kujiendesha kiueledi na wakiamini ujio wa Mohamed atakayeingia kwenye sejretalieti ya timu, utaongeza nguvu kwenye eneo la uongozi na hatimaye kufikia malengo waliyokusudia.

Azam FC inaamini katika uendeshaji mambo kiueledi ndani ya klabu  imekuwa na safu ya uongozi iliyosheheni watu wenye taaluma mbalimbali hivyo wanaamini kwa uzoefu aliokuwa nao Mohamed huko alikotoka akiwa kama Mwandishi wa habari kwenye shirika la utangaxaji (BBC) na nguvu kazi ya viongozi wengine utaweza kuifikisha Azam kwenye mafanikio