Na Prince Hoza
Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema yuko tayari kurejea Yanga endapo uongozi wa timu utafuata taratibu zote ikiwemo za kukubaliana na mwajili wake wa sasa TFF.
Akizungumza hayo leo, Mkwasa amesema Yanga inaweza kumrejesha kwakuwa ndiyo iliyomfikisha hapo, 'Nitarejea Yanga kama watanihitaji, siwezi kukataa naiheshimu sana Yanga kwani nimekuja Stars nikitokea Yanga hivyo siwezi kushindwa kurejea watimize taratibu tu', alisema Mkwasa.
Klabu ya Yanga inasemekana kwa sasa inataka kumrejesha kocha huyo hasa baada ya kuona haifanyi vizuri ikiwa chini ya Mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi kwani hadi sasa imeshacheza mechi sita za Ligi kuu bara ikiwa na pointi 11 wakati mpinzani wake Simba amecheza mechi saba lakini ana pointi 17 na anaongoza ligi huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Stand United yenye pointi 15.
Tayari Yanga imeshapoteza mchezo mmoja na ikiwa imetoka sare mechi mbili huku ikikabiliwa na mechi nyingine zenye ushindani, Katibu wa Yanga Baraka Deusdetit alipoulizwa kuhusu hilo akawa tofauti na kusema bado Yanga inawaamini makocha wake Pluijm na Mwambusi na kama itamuhitaji Mkwasa itaweka hadharani