Mavugo apewa mechi sita Simba

Na Saida Salum

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC  Laudit Mavugo raia wa Burundi, amepewa mechi sita na benchi la ufundi la timu hiyo na baada ya hapo atapigwa benchi kisha kutemwa msimu ujao.

Mavugo alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi za mwanzo mwanzo na kuishia kufunga mabao matatu tu na kujikuta akishindwa kufurukuta kwenye mechi zilizofuata na kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo.

Tayari Wanasimba walishaanza kumpenda na kumtukuza kama Emmanuel Okwi, lakini ameanza kupoteza ukali wake na sasa si lolote, chanzo cha habari kinasema, Mavugo amewaudhi Simba baada ya kushindwa kuifunga Yanga na sasa uongozi wa Simba unahaha kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Mganda Emmanuel Okwi anayecheza soka la kulipwa Denmark

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI