Manji awaita Wanayanga wote hata waliofukuzwa uanachama ili wamjadili

Kauli za Mwenyekiti YUSUPH MANJI leo kwenye Mkutano na waandishi wa habari.

"Kwenye mkutano mkuu baada ya mimi kuzungumza upande wangu, nitatoka nje ili wanachama wapate uhuru wa kujadili na kutolea uamuzi"

"Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano mkuu Jumapili waweze kuchangia masuala ya msingi kwa maendeleo ya klabu yao ila kama hujalipa ada ya uanachama kwa miezi 6 mkutano hautokuhusu"

"Ndani ya siku 90 baada ya kupewa ridhaa ya wanachama, tutaanza ujenzi wa uwanja wa mazoezi kwa timu"