Na Paskal Beatus, Dar es Salaam
BARAZA la wadhamini wla Klabu ya Yanga, limemkabidhi rasmi mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya Yanga Yetu, Yusuf Manji timu kwa muda wa miaka kumi kama alivyoomba kwenye mkutano wa dharula uliofanyika Agosti 6 mwaka huu.
Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu hiyo, amekabidhiwa timu leo mbele ya wadhamini wa klabu ambapo fomu ya makubaliano imesainiwa na kuanzia sasa Yanga ni mali ya Manji hivyo atakuwa akichukua asilimia 75 na wanachama wataambulia asilimia 25.
Ndani ya mkataba huo suala la uwanja limechukua nafasi kubwa pamoja na timu kushika nafasi mbili za juu, hivyo wachezaji wazurina bora watakuwa wakisajiliwa kwenye kikosi hicho ambacho juma lililopita kililazimishwa sare na watani zao Simba ya kufungana bao 1-1.
Yanga itakuwa imeandika historia ya kuwa klabu ya kwanza nchini kuendeshwa kikampuni kwani imefungua milango, Simba nao wako mbioni kumkabidhi timu mfanyabiashara kijana Mohamed Dewji