Na Patrick Sambai
Bondia mkongwe Mbaruk Heri anatazamiwa kuzichapa siku ya Jumamosi wakati michuano ya Goms Diwani Cup itakapofanyika katika uwanja wa Kampala uliopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mbaruk Heri ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa bondia maarufu nchini Mada Maugo, amesema yuko tayari kuzichapa na bondia yoyote atayejitokeza siku hiyo.
Michuano ya Goms Diwani Cup inafikia tamati siku ya Jumamosi kwa mechi ya fainali ya soka, pia kutakuwa na mashindano ya kuvuta kamba, kukimbia na gunia, kukimbiza kuku pamoja na ndondi.
Hatua ya nusu fainali inafikiwa kesho kwa timu za Talent na Quality kuumana vikali wakati kesho kutwa Black Wizard na Mazombi, michuano hiyo inaratibiwa na diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jakobo Kisi