Na Prince Hoza, Shinyanga
SIMBA SC jioni ya leo imeichapa Mwadui FC mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kwa ushindi wa leo Simba imefikisha pointi 32 na kuzidi kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi, mabao muhimu ya Simba yalifungwa na washambuliaji wake Mohamed Ibrahim 'Mo' aliyefunga mawili na Ramadhan Shiza Kichuya.
Simba imezidi kuiacha Yanga kwa tofauti ya pointi nane huku ikizidi kutimua vumbi