Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Kumbe yule jamaa aliyetobolewa macho na jambazi Scorpion, anayefahamika kwa jina la Said Ally Mrisho ni shabiki wa kutupwa wa Simba na ameweza kulia akiimbuka timu yake hiyo.
Said Ally amemwaga machozi hasa akiililia Klabu yake hiyo kwani hatoiona tena machoni mwake, Said anaikumbuka Simba kwani alikuwa akienda kuitazama lakini ndio basi hawezi tena kuiona Simba yake.
Anasema amewamisi wale mashabiki wakorofi waliong' oa viti uwanja wa Taifa Dar es Salaam, anakiri kama angekuwepo na yeye angeng' oa kwani ni mkerekwetwa haswa wa Simba, anawaomba mashabiki wenzake wa Simba wamuombee