Na Ikram Khamees
Siri zinazidi kuvuja, kumbe Kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio' wa Mwadui hajajiuzuru kama alivyosema, nasemekana kocha huyo mwenye maneno mengi kuliko wote amefutwa kazi baada ya mwenendo mbaya wa timu yake.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani ina uhakika nazo kwamba Julio amefutwa kazi na uongozi wa Mwadui ambao uko mbioni kupata kocha mpya na kilichobaki sasa ni kumpatia salio lake Julio.
Mwenendo wa Mwadui kwenye Ligi kuu bara si mzuri na ulimpatia mecho kadhaa kocha huyo na kufikia tamati, Julio alitangaza hadharani kwamba ameamua kujiuzuru ukocha kutokana na marefa kumuhujumu