Kocha mpya Yanga huyu hapa

Na Shafih Hoza

Yanga SC iliyokodishwa na kampuni ya Yanga yetu Limited, iko mbioni kumuajili kocha mkuu wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina ambaye tayari ana rekodi mbili tofauti ambazo zimewavutia Yanga.

Habari zilizotufikia hivi punde kuwa uongozi wa juu wa Yanga unataka kuachana na kocha wake wa sasa Mholanzi Hans Van der Pluijm hasa kwakuwa timu haifanyi vizuri ikiwa imeshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kitendo kinachowaumiza vichwa Wanayanga.

Lakini Hans Pluijm kama amewasikja viongozi wa Yanga kwani naye ameibuka na kusema anaanza ligi Alhamis ijayo Yanga itakapoikaribisha Mtibwa Sugar karika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Lwandamina ameivusha Zesco hadi nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, huku pia akiivusha timu ya taifa ya Zambia kwenye fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa nyumbani maarufu CHAN, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji anataka kuliondoa benchi lote la ufundi la Yanga na kumpa majukumu Mzambia huyo ambaye anakunwa na soka la Obrey Chirwa anayeozoea benchi Yanga