Kocha Mbeya City aigwaya Simba

Na Saida Fikiri, Mbeya

Kocha mkuu wa Mbeya City, Mzambia Kinah Phiri ameonyesha kama anaigwaya Simba baada ya kusema kwa sasa ina kikosi kizuri lakini kamwe hatotishika na amepanga kujinyakulia pointi tatu.

" Sina shaka sana na mechi ya Jumatano dhidi ya klabu ya simba kwani aina ya mpira wachezao Hauna tofauti sana na Huu wa kwetu ,  Nia yetu ni kuibuka na point 3 muhimu kwani nawajua vizuri simba na nina matumaini tele ya kuondoka na Ushindi "

" Wachezaji wangu wamesema wapo tayari kwa mapambano na kila mmoja akisema lazima simba afungike hapa ,  Najua simba iko vizuri kwa sasa ila dakika 90 Zitaongea kwani Iliniuma sana kuambulia point 1 mbele ya stand United ikiwa tuliwakamata kila idara ila Nimeliona tatizo na nimelifanyia kazi "

Hayo ni maneno ya kocha mkuu wa klabu ya mbeya City ,  Mzambia