Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini la Klabu ya Yanga, Francis Mponjoli Kifukwe amempasha katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja kuwa uamuzi wa kuikodisha timu kwa Yusuf Manji umefuata taratibu zote na wala hawakukosea.
Kifukwe amedai wao walifuata kila kitu kwa kufuata mwongozo kwa wanasheria wao wazoefu kama John Mkwawa na Alex Mgongolwa ambapo wakajiridhisha na kuamua kusaini mkataba wa kuikodisha Yanga kwa kampuni ya Yanga Yetu LTD iliyo chini ya Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa Yanga SC.
Kiganja alitakiwa kuuandikiwa barua uongozi wa Yanga ili kuomba ufafanuzi na si kuropoka kwenye vyombo vya habari kama alivyofanya, amedai wao hawazuiwi na baraza hilo ila baraza hilo linaweza kuwataka wabadili vipengele kama wameona hivyo