Kichuya awa mchezaji bora Simba

Na Prince Hoza

Winga na kinara wa mabao Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Shiza Ramadhan Kichuya, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Septemba mwaka huu.

Kichuya ambaye ndiye kinara wa mabao Ligi kuu bara akiwa amefunga mabao sita, ameshinda tuzo ya uchezaji bora wa mwezi Septemba akiwa amefanya vizuri na kuiwezesha timu yake ya Simba kuongoza Ligi.

Kufanya vizuri kwa nyota huyo kumenfanya awe mwanasoka bora, Kichuya aliyesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani Manungu wilayani Mvomelo mkoani Morogoro kwa sasa ndiye mchezaji anayeng' ara