Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo inawakaribisha Mbao.FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi kuu Bara uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mbao ambao katika siku za hivi karibuni imekuwa katika kiwango kizuri ikizitoa nishai timu ilizokutana nazo, hivyo hata katika mchezo wake na Simba leo unatajwa kuwa na ushindani.
Simba ambayo ndiyo vinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 23 inatarajiwa kujiongezea pointi nyingine tatu ingawa si kirahisi mno kama inavyodhaniwa na mashabiki wake.
Baada ya mchezo wa leo, Simba inajiandaa na mchezo mwingine dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika uwanja huo huo wa Uhuru, nyota Shiza Kichuya anatarajia kuonyesha tena cheche zake kama kwenye michezo iliyopita wakati timu hiyo ikitoa vipigo