Hanspoppe aunga mkono mashabiki kung' oa viti Taifa

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC, Zacharia Hanspoppe ameshangazwa na wale wote wanaokosoa kitendo cha mashabiki wa Simba kufanya vurugu kwa kung' oa viti.

Hanspoppe akizungumza na chombo kimoja cha habarj (Siyo hiki) alisema ni bora kung' oa viti kuliko kung' oa meno ama vurugu nyingine ambazo zingelepelea madhara kwa mtu/watu.

Kigogo huyo wa usajili amesema mwamuzi wa mchezo Martin Saanya ndiye aliyepaswa kubebeshwa lawama kwani yote yamesababishwa na yeye, "Mtu anauchukua mpira na mkono halafu anafunga goli, refa anakubali, huoni kama ni uvunjifu wa amani mbele ya maelfu ya watazamaji" alisema Hanspoppe