Picha/Habari na Prince Hoza
Kituo cha utangazaji cha Sibuka Fm, Jumamosi ilikinukisha katika mitaa ya Tabata Mtambani ikiunguruma na kipindi chake kimoja cha michezo ya wiki kinachojulikana kama MBS kikiongozwa na mtayarishaji wake David Pasko.
Kipindi hicho cha masaa mawili kilifana kwani watu wengi wakiwemo wadau wa michezo walijitokeza, pia wachezaji wa zamani nao walipata nafasi ya kuzungumzia machache kuhusu mchezo wa soka.
Naye mtangazaji wa kipindi hicho David Pasko amesema huo ni utaratibu wa redio yao kuwafikia wasikilizaji wake kila mahari, amesema kila Jumamosi watatembelea maeneo mbalimbali kuhakikisha wanawafikia wadau wao pia kujua maendeleo ya soka nchini na sehemu husika
