Na Ikram Khamees, Morogoro
Kama ulikuwa haujui basi sikia hii. Goli lililofungwa dakika ya 26 kipindi cha kwanza na mshambuliaji hatari Amissi Tambwe raia wa Burundi na kuiandikia Yanga bao la kuongoza limesababisha kifo cha mshabiki wa Simba wa Dumila mkoani Morogoro.
Shabiki huyo ambaye pia ni mwanachama, alipatwa na mauti baada ya kuanguka kwa presha wakati Tambwe akifunga bao hilo katika uwanja wa Taifa, Dar esSalaam.
Mwandishi wa mtandao huu alizipata taarifa za shabiki huyo aliyeaga dunia ambaye alisafiri hadi Dar es Salaam kuhushuhudia mwenyewe mtanange huo,lilipoingia goli hilo, shabiki huyo alianguka kwa presha lakini baadaye akaanza kujisikia vizuri na kulazimika kurejea kwao Morogoro.
Lakini kwa bahati mbaya akazidiwa ghafla na kufariki dunia huku chanzo kikidaiwa ni goli la Tambwe, Yanga na Simba zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa, Dar es Sallaam