Chirwa mtamkoma wenyewe, aifungia mabao mawili Yanga ikiifunga Kagera Sugar 6-2

Na Saida Salum, Bukoba

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc Jumamosi wamefufua matumaini baada ya kuichabanga bila huruma Kagera Sugar kwa mabao 6-2 Uwanja wa Kaitaba mchezo wa Kigi kuu Bara.

Mshambuliaji aliyekuwa akibezwa sana na vyombo vya habari, Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao mawili peke yake wakati Mzimbabwe Donald Ngoma naye akifunga mawili.

Magoli mengine ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke na Simon Msuva na kuifanya Yanga itoke na ushindi mnono huku ikifikisha pointi 21 ikiendelea kushikilia nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya Stand United ambayo ililazimishwa sare 3-3 na Mtibwa Sugar.

Mabao ya Kagera yalifungwa na Mbaraka Yusuphu, mechi nyingine kama ifuatavyo.

Mtibwa Sugar 3 Stand United 3, African Lyon 2 Mbeya City 0, Majimaji 1 Ruvu Shooting 1, Ndanda 1 Mwadui Fc 2, Jumapili Simba itaikaribisha Toto Africans uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam