Na Salum Fikiri Jr, Mwanza
Viungo washambuliajj Obrey Chirwa raia wa Zambia na Saimon Happgody Msuva, jana jioni kila mmoja alifunga bao moja, Yanga SC ikiwazamisha wadogo zao Toto Africans 'Wana kishamapanda' mabao 2-0 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mchezo wa Ligi kuu Bara.
Ushindi huo wa Yanga uliwafanya wafufue matumaini ya kuifukuzia Simba inayoongoza ligi hiyo, Yanga imefikisha pointi 18 ikiwa imeshuka dimbani mara 8, Chirwa alifikisha bao lake la pili tangu ajiunge na Yanga akitokea FC Platinum mwishoni mwa Julai.
Goli hilo lilipatikana kipindi cha kwanza, kipindi cha pili Yanga wakaongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa kistadi na Saimon Msuva, Matokeo mengine Prisons 2 Stand United 1, Mbeya City 1 Ndanda 1, Majimaji 2 African Lyon 0, Ruvu Shooting 1 Mwadui 1, na Azam FC 1 Mtibwa Sugar 1, leo Simba inacheza na Mbao ya Mwanza uwanja wa Uhuru