Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Hali si shwari kwenye timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam hasa kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo katika Ligi kuu ya Tanzania bara inayoendelea ambapo hadi sasa imefikisha pointi 11 ikiwa imecheza mechi 8.
Mabingwa wa Klabu Afrika mashariki na kati wameshapoteza mechi tatu, Jana Azam imelala bao 1-0 na Stand United katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Tayari Azam ilishafungwa na Ndanda FC mabao 2-1, Simba SC 1-0 na jana ikapoteza mchezo mwingine tena dhidi ya Stand, matokeo hayo yameifanya Azam ishikilie nafasi ya tisa ikiwa na pointi 11 ikicheza mechi nane.
Hofu imemkumba nahodha wa timu hiyo John Bocco "Adebayor" yuko hoi akiwa na wasiwasi mkubwa kwani yeye alishatakiwa aondolewe kikosini na makocha wapya wa timu hiyo ambao ni raia wa Hispania, Bocco huenda akaachwa kutokana na ripoti ya kocha huyo itakapowasilishwa kwa uongozi kwakuwa hadi sasa hajafanya lolote