Na Mwandishi Wetu
Nahodha wa zamani wa Togo na mshambuliaji wa timu za Arsenal na Tottenham zote za England, Emmanuel Adebayor, ametamba kumkingia kifua beki na nahodha wa sasa wa timu ya taifa ya Togo, Vincent Bossou.
Bossou ambaye pia ni beki tegemeo wa mabingwa wa soka Tanzania bara ameahidiwa kutafutiwa timu barani Ulaya na Mtogo mwenzake aliyewahi kutamba barani ulaya, Adebayor amesema atajitahidi kuhakikisha Bossou anapata timu msimu huu ama ujao.
Naye beki huyo ametoa tamko kwamba yuko tayari kwenda Ulaya kama atapatiwa timu na Adebayot, lakini kama hajapata timu Ulaya basi ataendelea kuitumikia Yanga kwani ndiyo timu iliyomsukuma mpaka kufikia hapo halipo