Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Wawakilishi pekee wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Yanga SC, jioni ya leo imepata ushindi wa kwanza tangia kuingia hatua ya makundi, baada ya kuilaza MO Bejaia ya Algeria bao 1-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi wa leo umeifanya Yanga kufikisha pointi 4 na sasa itasubiriwa miujiza katika mchezo wake wa mwisho ili iweze kutinga Nusu fainali, Licha ya kupata ushindi huo mwembamba, Yanga ilikosa magoli mengi kupitia kwa Obrey Cholla Chirwa ambaye alipoteza nafasi tatu za wazi.
Yanga iliandikisha bao la kwanza na la ushindi lililofungwa na mshambuliaji wake mahiri Amissi Tambwe ambaye aliunganisha mpira wa adhabu iliyopigwa na Juma Abdul, kipa wa Yanga Deogratus Munishi 'Dida' alionyesha uwezo mkubwa licha ya kuumizwa mara kwa mara na wachezaji wa MO Bejaia