Yanga yabutuliwa 3-1 na TP Mazembe

Na Ikram Khamees, Lubumbashi

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC, imemaliza ushiriki wake wa kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya kupokea kichapo cha mshangao cha mabao 3-1 toka kwa mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya Lubumbashi.

TP Mazembe ambao tayari wamefuzu Nusu fainali, lakini wakataka kuweka heshima kwa kuwafunga mabingwa wa Tanzania bara Yanga, magoli ya TP Mazembe iliyofikisha pointi 13 yaliwekwa kimiani na Rayfred Kalaba aliyetupia mawili na Bolingi aliyefunga moja.

Yanga walipata bao lao la kufutia machozi lililofungwa na straika wake hatari Amissi Tambwe ambaye pia ni mfungaji bora wa Ligi kuu bara, Yanga sasa wanarejea Tanzania ambapo Jumapili wataanza kampeni yao ya kutetea ubingwa wa bara watakaposhuka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mechi yao ya kwanza