Yanga waapa kufia Taifa Jumamosi

Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, wameapa kufia uwanjani Jumamosi watakapoikaribisha MO Bejaia ya Algeria katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kundi A.

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ameiambia Mambo Uwanjani kuwa ni lazima waibuke na ushindi katika mchezo huo kwani wanahitaji pointi tatu.

Endapo Yanga itapata ushindi itafufua matumaini ya kusonga mbele kwani itafikisha pointi nne ingawa itaendelea kushikilia mkia, Yanga ndio timu pekee kwenye kundi hilo ambayo haijaonya ushindi ikiwa imepoteza mechi tatu kati ya nne ilizocheza