Yanga na MO Bejaia hatumwi mtoto dukani

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Mabingwa wa soka wa Tanzania bara Dar Young Africans (Yanga), jioni ya leo inashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwavaa wageni wao Moulodia Olympic Bejaia ya Algeria mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi.

Yanga inataka kulipiza kisasi baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Algeria, lakini pia inataka kupata ushindi wake wa kwanza ili ijinasue kutoka mkiani mwa kundi A, Yanga imevuna pointi moja pekee ambapo ijishinda inaweza kupanda kidogo.

MO Bejaia wenyewe nao wanataka ushindi kwani hadi sasa wamefikisha pointi tano na kama wakishinda watafikisha pointi nane na kujihakikishia nafasi ya kutinga Nusu fainali