Yanga kusaka heshima leo Taifa

Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam

Mabingwa wa soka wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga SC, jioni ya leo inajitupa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwavaa African Lyon.

Huu unakuwa mchezo wa kwanza wa Yanga ambao wanakumbukumbu mbaya baada ya kufumuliwa mabao 3-1 na Tp Mazembe mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mabingwa hao watetezi waliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kumaliza kwenye kundi A wakiwa na pointi nne huku Tp Mazembe ikimaliza ya kwanza na Mo Bejaia ikishika ya pili na kusonga mbele.

Hivyo Yanga wataingia uwanjani leo wakiwa na hasira ya kutolewa na kuhitaji matokeo mazuri ili waweze kuwafurahisha madhabiki wao, endapo itapata ushindi itafikisha pointi tatu, Lyon wao wameshacheza mechi moja dhidi ya Azam FC ambayo walitoka sare ya kufungana 1-1