Yanga kurejea kwenye anga zake VPL

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

YANGA SC sasa imetangaza kiama kwa wapinzani wake baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, mabingwa hao watetezi wameichimba mkwara African Lyon ambayo watakutana nayo Jumapili ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusidetit ameiambia Mambo Uwanjani kuwa Yanga inewasili nchini ikitokea Lubumbashi ambako ilitolewa rasmi katika michuano ya Shirikisho kwa kufungwa mabao 3-1 na wenyeji wao Tp Mazembe ya DR Coongo.

Deusdetit amedai Yanga inarejea kwenye anga zake za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) hivyo timu yoyote itakayokatiza mbele yao wataipa kisago, Yanga Jumapili ijayo itakutana na African Lyon hivyo wanaanzia katika mchezo huo na kuendeleza kwa JKT Ruvu ambao watakutana nao Jumatano ijayo