Badala ya akina Joti, Elia Daniel naye shakani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jeshi la polisi nchini linawasaka wasanii wa kundi la Orijino Komedi linalowahusisha wasanii Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), Joti na Mac Regan kwa kosa la kuvaa sare za polisi kinyume cha sheria.

Wasanii hao walitinga sare hizo wakati wa sherehe ya harusi ya msa ii mwenzao Masanja, inasemekana wasanii hao wakivaa sare hizo za polisi, hata hivyo wasanii hao walikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa masaa kadhaa isipokuwa Masanja bado anaendelea kutafutwa.

Wimbi la wasanii kuvaa sare za polisi linazidi kukithiri, si mara ya kwanza kwa wasanii hao kuvaa sare za polisi kwani mwaka juzi msanii Diamond Platinum alidakwa na polisi kwa kuvaa sare za JWTZ, ukiachana na hao, wapo wasanii wengine wanaoshiriki katika sanaa zao wakiwa wanatumia silaha kama hapo (Pichani)