Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Pamoja na klabu ya Simba kusisitiza mshambuliaji wake mpya, Laudit Mavugo ni mali yake, Vital'0 ya Burundi imeendelea kusisitiza bado inammiliki.
Vital'0 imetuma jina lake kwenye Shirikisho la soka la Burundi (BF) ikiwa ni sehemu ya wachezaji itakaowatumia msimu ujao.
Hali hiyo inaashiria mgogoro wa usajili kwa Mavugo ambaye amejiunga na Simba msimu huy akielelezwa kumaliza mkataba na timu yake hiyo ya zamani.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema Mavugo hana tatizo lolote la usajili, "Ni mchezaji wa Simba na hakuna maelekezo mengine zaidi", alisema.
Lakini Rais wa Vital'0, Benjamin Bikorimana amesema Mavugo hajamaliza mkataba na timu yake kama inavyoelezwa.
"Ni kitu cha kushangaza sana, Simba wanapoteza muda, ITC yake ipo kwetu, huyu ni mchezaji wetu na tuna mkataba naye Simba wanajisumbua", alisema Bikorimana